Album “NASHUKURU” by Ezekiel Kwizera (Burundi Gospel)

By  |  0 Comments

Eze Album

 

Ezekiel Kwizera ni mwana Gospel Musician kutoka Sioux Falls, South Dakota, USA. Mwana musik huu ametoa mkanda (alubamu) wake wa kwanza ambao unaenda kwa Jina NASHUKURU. Tulifanikiwa kuongea naye baada yake kutangaza kua alubamu yake ya kwanza kufunguliwa rasmi. Muimbaji huu wa Gospel anasema kwamba umekutana na changamoto mbalimbali hadi kufikia hatua ya kuaza kusimamisha kazi ya kurikodi kutokana na ugumu pia na majaribu. Lakini kasema kua Mungu amemusaidia sana akamuezesha kuendeleza bidii ya kurikodi hadi akamaliza. Mwenyewe alijitengenezea beats na akajilikodi masauti mwenyewe, pia na ku mix nyimbo hizo, kazi zote hizo zilichangia kumpa changamoto kadharika.

Muimbaji Ezekiel Kwizera amesema kua lengo lake kuu kufanya alubamu hii ni kwamba siku nyingi alikua anapuuzia wito wa Mungu, lakini siku moja wakiwa katika chumba cha maombi, sauti ikasikika kwamba kuna mtu kati ya waliopo kwenye chumba hicho cha maombi ambae amekataa kusikia wito wa Mungu. Muimbaji Eze Kwizera alipo sikia sauti hiyo, maramoja akajua kua ni yeye. Ndipo akawa makini sana kwa kumtumikia Mungu. Jina la alubamu hii “NASHUKURU”, Muimbaji Eze anasema kama aliamua kuita alubamu hii hilo jina kwa kumushukuru Mungu alipo mtoa na alipo mfikisha, Maana ni neema ya Mungu.

Ujumbe mkuu ambao Muimbaji Eze anatarajia wadau na wasikilizaji kupata ni kwamba kwa kila jambo lote lile mwanadamu anapitia, ikiwa shida, hali mbaya, na majaribu kadharika, inatupasa Tumushukuru Mungu na Kumwabudu, maana utukufu wote unabaki kua wake daima na tusisahau kua Mungu yuko upande wetu kila siku.

Mkanda huu wa CD, unapatikana kwenye address hii 6057282550, 6057281376!
Sioux Falls South Dakota USA na mnaweza kupigia muimbaji huo katika namba ifuatayo: 6052517130

Muimbaji Eze anasema kua anafikiri kutoa Video ya Alubamu hii tena wadau na mashabiki watarajie kupata nyimbo na alubamu nyingi kutoka kwake. Anaomba msaada kwa wasikilizaji na wadau wa nyimbo za injili, ili akaweze kuendelea kufanya kazi kama hizi, muhimu zaidi anaitaji maombi. Kununua mkanda huu itakua moja wapo wa ku support kazi zake, twawasihi kununua mkanda huu ili mpate ujumbe kutoka kwenye CD hii.

 

Share
Profile photo of Burundian Gospel

Share

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

error: Copyright reserved by The Shemeza Co. ©2017
Skip to toolbar